Kiswahili

How to vote correctly (Swahili)

Video transcript

Hello, jina langu ni Winta. Mimi ni Balozi wa Demokrasia.

Ninafanya kazi katika Tume ya Uchaguzi ya Victoria.

Uchaguzi katika Jimbo la Victoria utafanyika Novemba. Ili kura yako ihesabiwe, lazima ukamilishe karatasi zako za kupigia kura kwa usahihi.

Ile ndogo ni ya Nyumba (Baraza) ya Chini.

Ile kubwa ni kwa Nyumba (Baraza) ya Juu.

Tuanze na Nyumba (Baraza) ya Chini. Tumia nambari wakati wa kupiga kura.

Inaweka namba kwenye masanduku yote kwa mpangilio wa chaguo yako.

Weka nambari 1 karibu na mgombea ambaye unataka kuchaguliwa zaidi

Weka nambari 2 karibu na chaguo lako la pili

Weka namba 3 karibu na chaguo lako la tatu na kadhalika

Lazima uweke namba kwa kila sanduku.

Ili kupigia kura Baraza la Juu, una njia mbili.

Njia ya 1 - Juu ya mstari

Uweke nambari 1 kwenye kisanduku karibu na chama au kikundi unachotaka kushinda zaidi. Ukifanya hivi, chama au kikundi unachochagua kitaamua ni wagombea gani watapata kura yako.

Kisha umemaliza.

AU

Njia ya 2 - Ikiwa unataka kuchagua wagombeaji wewe mwenyewe badala ya chama au kikundi kukufanyia, piga kura chini ya mstari.

Lazima uweke angalau masanduku 5 kwa mpangilio wa chaguo yako.

Weka nambari 1 karibu na mgombea ambaye unataka zaidi ashinde.

Weka nambari 2 karibu na chaguo lako la pili.

Weka nambari 3 karibu na chaguo lako la tatu.

Weka namba 4 karibu na chaguo lako la nne.

Weka namba 5 karibu na chaguo lako la tano.

Ikiwa unataka, unaweza kuendelea kuhesabu visanduku zaidi au vyote.

Ukishajaza karatasi zako zote mbili za kupigia kura, unahitaji kuziweka kwenye masanduku ya kura kwa kila moja.

Ikiwa unahitaji usaidizi wowote siku hiyo, unaweza kuleta mwanafamilia au rafiki wa kukusaidia. Unaweza pia kuuliza mfanyakazi wa VEC.

Ikiwa una maswali yoyote au ungependa usaidizi, tafadhali piga simu 9209 0112 nambari ya huduma ya mkalimani au tembelea tovuti yetu vec.vic.gov.au na uchague nembo ya mkalimani.

Uchaguzi katika Jimbo la Victoria utafanyika Novemba. Raia wa Australia pekee ndio wanaoweza kupiga kura katika uchaguzi huo. 

Ikiwa umejiandikisha kupiga kura, lazima upige kura.